Klabu za Utu
Karibuni rafiki! Kama mnavyofahamu, watoto wa Ubongo Kids ni wadadisi na washirikiana sana, wanajifunza, wanakua na kuboresha maisha yako. Wana kaulimbiu yenye nguvu sana iitwayo UTU ambayo inabeba msingi wa maadili yao na vitu wanavyotaka kufikia katika ubinadamu, kusaidiana, kupenda na kujali watu pamoja na mazingira yanayowazunguka.
Kwenye wavuti hii, utapata vipindi kutoka Msimu wa 5 wa Ubongo Kids ambao unazingatia sifa za UTU na miongozo wa kusaidia kuwezesha usajili wa Vilabu vya UTU katika jamii au shule zako. Kupitia kusikiliza vipindi, watoto watajifunza jinsi ya kuonyesha UTU, kuboresha ustawi wao na jamii zao.
Kila kipindi huja na malengo ya kujifunza. Baada ya kila kipindi, kutakuwa na maswali kwa watoto kujadili na pia masuala ya UTU wanayoweza kufanya. Mwongozo wa kilabu cha UTU pia utaangazia ujumbe mkuu au lengo la kujifunza la kila kipindi.
Hii itakuwa njia ya kufurahisha, ya mwingiliano kwa watoto kujenga maarifa na ustadi katika STEM, kufanya vizuri katika jamii yao na kufanya kazi pamoja kuonyesha UTU.
Vipindi Vipya
Nguvu ya uvutano
(Shukrani)
Mimi ni yule yule
(Ujasiri)
Uwajibikaji
Usawa
Ukarimu
Unyenyekevu
Kuelewa anachopitia mwingine
Sajili klabu yenu leo
Imedhaminiwa na