Siku ya Binti Duniani

11 Octoba ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike na Ubongo Kids hawawezi kukaa kimya. Wanataka kuungana katika kuelimisha kwa ajili ya siku hii ya muhimu na kutangaza dhima ya: “Msichana aliye na ujuzi.”. Kwa siku za hivi karibuni vijana wenye ujuzi wanahitajika zaidi kuliko wakati mwingine kwenye makampuni za kifumbuzi. Hata hivyo, robo ya vijana duniani kote (zaidi mabinti) hawana ajira. Elimu ni muhimu sana kwa maandalizi ya vijana kwa ajili ya ajira duniani, lakini duniani kote, zaidi ya wasichana millioni 130 wenye umri wa kwenda shule hawasomi shuleni.

Wasichana watatu wenye matumaini makubwa ya kutumia ujuzi na vipaji vyao kwa ajili ya ajira zao za kesho ni Kiduchu, Kibena na Amani. Wasichana hawa kutoka Kokotoa wanataka kushirikisha ndoto zao kwa dunia ili kuweza kuhamasisha kizazi cha wasichana wa sasa wanaojiandaa kuingia kwenye dunia ya kazi:

Amani

“Ndoto yangu ni kutumia sauti yangu kuleta matokeo. Kuimba ni ujuzi ambao nimechagua kutumia kwa sababu mziki una vuka mipaka ya lugha na utamaduni na pia unaleta watu pamoja bila kujari ni kina nani au wanaonekanaje”

Kibena

“Nataka kazi ambayo inasaidia watu na kutoa kwa jamii. Ningeweza kuwa daktari, mwalimu au kufanya kazi za kijamii, uwezekano hauna mwisho! Natazama mbele kwa ajili ya yajayo mbele yangu”

Kiduchu

“Kama Msichana mwenye kuthubutu nina ndoto ya kuwa mtu wa kwanza kutoka Kokotoa kuwa mnajimu. Nina vutiwa na anga na ninataka jina langu kuwa kati ya wanawake waliofanikiwa katika kazi yangu ambayo ina wanaume zaidi.”

Koba na Baraka

“Wasichana wana matarajio kama vile wavulana lakini wana nafasi chache kuyatimiza kupitia elimu. Sio haki! Tusimame pamoja nao kubadirisha habari hii” – Koba

“Nimewahi kufikiria kuwa kuna kazi za wavulana na wasichana lakini baadaye nikagundua kuwa wasichana wanaweza kufanya chochote wanachoweza kufanya!” – Baraka

 

Angalia Video Maalum kwa Siku ya Binti Duniani: