Simamia Fedha Zako: Walivyosema Watazamaji Wa Ubongo Kids!

Vijana wa kitanzania hasa wasichana- wanakosa elimu ya fedha. Lakini elimu ya fedha ni nini? Ni ujuzi unaokusaidia kuelewa jinsi fedha inavyofanya kazi na pia inakusaidia kujenga tabia nzuri ya matumizi ya fedha, kama vile kuweka akiba au kutengeneza bajeti. Ukiwa na ujuzi huu utakuwa na uwezo wa kudhibiti hela yako maisha yako yote. 

Hapa Ubongo, huwa tunaangalia njia za kuwasaidia vijana kama WEWE kukua na kufanikiwa. Kwa kushirikiana na DLI na Spring tuligundua kwanini wasichana wanakosa elimu ya msingi ya fedha na kuona namna Ubongo inavyoweza kufanya kuhusu jambo hili. Ili kufahamu wasichana wanafikiria nini kuhusu fedha, tulisafiri mpaka vijiji vya Nakuru (Kenya), Mwanza na Shinyanga (Tanzania).  Wasichana tulioongea nao walikuwa wakipewa hela ya matumizi ambayo waliitumia kununua pipi na chipsi kama watoto wengine wanaoishi mjini. 

Baada ya hapo, muda wa kuwa wabunifu ukawadia! ! Tukatengeneza vipindi  vipya vitatu  kufundisha ujuzi muhimu wa matumizi ya fedha: akiba, jinsi ya kupata kipato na kupanga bajeti. Kwenye vipindi hivi, wasichana wenye ujasiri wanaanzisha kikundi cha kuweka akiba, wanatafuta njia sahihi na salama za kupata kipato na kutumia “Ubongo” kupanga bajeti. 

Lakini hatukuishia hapo- tulitaka kupata maoni kutoka KWENU, watazamaji wetu! Mwishoni mwa kila kipindi tulikukaribisha utupe mawazo yakokuhusu fedha na ajira. Majibu tuliyoyapokea yalikuwa mazuri sana. Watu kama 700 hivi walitoa mawazo yao kila wiki. Kusema ukweli, majibu yenu yalikuwa yanavutia sana. Tuliamua kutengeneza video fupi kwa ajili yenu wote. 

https://www.youtube.com/watch?v=7a1nmFK5qtI&t=68s

https://www.youtube.com/watch?v=4VCyWoENB-U&t=0s&index=15&list=PLjSFjqcCS3M9heNXzyDl_5UNexNsWTtO1

https://www.youtube.com/watch?v=yz46BOHUUD0&t=126s

Hivi ndivyo mlivyosema… 

Akiba (unahifadhi wapi fedha zako?)

Kipato (unapata wapi fedha zako?)

Wengi wenu mlisema kwamba elimu ni muhimu na  kwamba mnaweka akiba ya fedha kununua vifaa vya shule au kwa ajili ya malengo ya kielimu. Pia, wengi wenu mlituambia njia mnazotumia kuweka akiba, na ikaonekana kwamba wengi mnatumia akaunti ya benki kuweka akiba.. 

Pia tulitaka  kuelewa jinsi watazamaji wetu wanavyofanya maamuzi ya kiwango cha kuweka akibana kiasi cha kutumia; hivyo tuliwauliza kama mnapanga bajeti. Asilimia 80 ya watu walisema wanatumia bajeti kupanga matumizi yao ya fedha. 

Bajeti (unapangilia vipi fedha zako?

Tulipenda sana kusikia kuhusu matumizi yenu ya fedha na tunathamini maoni yote tuliyoyapokea. Hii inaonyesha jinsi elimu ya fedha ilivyo muhimu kwa KILA MMOJA: inatusaidia kuwa na matumizi mazuri ya fedha kila siku na kufikia malengo yetu ya baadaye. Tunatumaini kwamba tutaendelea kukusanya maoni mengi zaidi kutoka kwa watazamaji wetu  na kutengeneza vipindi vingi vitakavyowasaidia kujifunza na kufanikiwa.