Kibena

Huyu ni Kibena. Ana miaka 10 na ni rafiki mzuri kwa kila mtu. Linapotokea tatizo lolote yuko tayari kusaidia. Anaishi na Bibi anayemtia moyo kufanya vizuri – si jambo la kushangaza kuwa anashika nafasi ya juu darasani!

Jina: Kibena Nambari
Umri: 10
Familia: Bibi na mama (anayeuza chapati mjini)
Anachoopenda: Kusoma
Anachochukia: Pale ambapo rafiki zake wanataka kumuigilizia majibu ya jaribio darasani
Siri kubwa: Aliwahi kufuga sungura wadogo watano chini ya kitanda chake kwa miezi mitatu bila bibi yake kujua! Walikuwa peke yao kwahiyo ilibidi awasaidie!

Tazama Video za Kibena Kupaka Rangi

Kiduchu

Kiduchu ana miaka 11. Huwezi kumkosa na nywele zake za kipekee! Anapenda kufikiria kuwa yeye ni bosi, lakini kuna wakati anasahau kufikiri kabla ya kutenda hivyo kusababisha matatizo kwake na kwa rafiki zake. Wakati hachezi mpira au kuwa kwenye matukio ya kufurahisha ya Ubongo Kids, huwa anapanga kusafiri kwenda angani kama mnajimu mwanamke wa kwanza wa Afrika!

Jina: Kiduchu Sila
Miaka: 11
Familia: Mama, baba na kaka
Anachopenda: Mchezo wowote hasa mpira wa miguu na danadana!
Anachoochukia: Watu wanapomwambia abadilishe nywele zake
Siri kubwa: Alishawahi kuvaa kama mvulana ili aweze kucheza mpira wa miguu kwenye mechi ya wavulana – na akashinda!

Tazama Video za Kiduchu Kupaka Rangi

Koba

Koba ana miaka 11, ni mtengenezaji wa filamu na kaka kwa Baraka na Mwenda. Anaweza kulalamika kwa rafiki zake, lakini kusema kweli anapenda majukumu yake ya kuwa kaka mkubwa kisirisiri. Pia Koba anajaribu kuwa jeshi la mtu mmoja katika jamii yake, iwe katika kuleta umeme shuleni au kuanzisha bustani ya jamii.

Jina: Koba Chimo
Umri: 11
Familia: Mama, mdogo wake wa kiume (Baraka) na mtoto mdogo wa kike (Mwenda)
Anachopenda: Kutengeza filamu
Anachochukia: Baraka anavyokoroma akilala
Siri kubwa: Amewahi kuiba pipi za Baraka wakati Baraka haangalii

Tazama Video za Koba Kupaka Rangi

Baraka

Baraka ndio mtoto mdogo kuliko wote wa Ubongo Kids na anajua hilo! Kila wakati anatafuta njia za kumfanya akue na anapenda sana utani (mara nyingine anapata shida sana kueleweka na watu kwa sababu wamezoea utani wake!). Baraka ana maswali mengi na hakati tamaa mpaka amepata majibu anayoyatafuta. Hali hiyo humfanya kuwa msumbufu kidogo.

Jina: Baraka Chimo
Miaka: 9
Familia: Mama, Kaka mkubwa (Koba) na mdogo wake (Mwenda)
Anachopenda: mpira wa kikapu
Anachochukia: kuambiwa nini cha kufanya
Siri kubwa: analala na picha ya Nelson Mandela chini ya mto wake akitumaini kwamba siku moja atakuwa Rais

Tazama Video za Baraka Kupaka Rangi

Amani

Kutana na Amani – ana miaka 10 ni binti mwenye ulemavu wa ngozi na ana kipaji kikubwa cha kuimba kuliko waimbaji wote wa Kokotoa (hatuna shaka na hilo!). Ni binti mzuri na anayejali, lakini wakati mwingine anatumia muda mwingi sana kwenye kazi yake ya muziki na anasahau kazi za shule. Kama Amani atashindwa kupata wimbo wa kutatua tatizo lako, basi atawaita rafiki zake wamsaidie.

Jina: Amani
Familia: Baba na dada mkubwa
Anachopenda: Kuimba
Anachochukia: Kusafisha sehemu ambayo watu wamechafua
Siri kubwa: Ana kitabu cha siri anachoandika nyimbo kuhusu rafiki zake

Tazama Video za Amani Kupaka Rangi

Nina

 

Name: Nina
Age: 12
Family: Anaishi na mjomba na shangazi yake ambao ni madaktari.
Favourite Hobby:  Kusoma / Kujifunza vitu vipya.
Hates it when: Kula nyama. (anapendelea kula mboga mboga tu)
Biggest Secret: Bado.

Tazama Video za Nina Kupaka Rangi

Mama Ndege

Kama unatafuta ndege mwenye busara na bingwa wa hisabati, basi usiendelee kutafuta! Mama Ndege ni mama wa msituni na mkali wa hisabati. Yuko tayari kutoa ushauri kwa jambo lolote, na ana tabia ya kuzuka tu na kukusaidia wakati ambao humtegemei kabisa! Ni shabiki mkubwa wa nyimbo na kucheza, na ana kicheko cha kuvutia, Kokotoa nzima hakuna! Kama Mama Ndege hawezi kukufanya ucheke basi hakuna mwingine atakayeweza!

Jina: Mama Ndege
Umri: 60 (umri wa ndege)
Familia: Makina mawili mapacha
Anachopenda: Kutengeneza nyimbo za hisabati
Anachochukia: Watu wanavyomtenga kwa sababu yeye ni ndege
Siri kubwa: Hapendi kuzeeka na kusahau mambo kwahiyo anajaribu kufundisha watu ujuzi wake, kama likitokea lolote awe tayari!

Tazama Video za Mama Ndege Kupaka Rangi

Anko T

Yeyote anayesema twiga hawezi kufanya mziki wa kufokafoka basi hajawahi kutana naAnko T! Ni mrefu kuliko rafiki wote wanyama, na yuko tayari kughani mistari mikali ya mada yoyote unayopenda. Lakini usidanganyike, ana roho nyepesi sana! Ingawa anaweza kutoa msaada kwa rafiki zake wa msituni na wa Ubongo Kids, yeye anaona aibu sana kuomba msaada kwa wenzake.

Jina: Anko T
Miaka: 41 (umri wa twiga)
Familia: Wanyama wote! (Aliasiliwa na wanyama wakubwa wa mwituni kwani alitelekezwa akiwa mdogo sana)
Anachopenda: Muziki wa kufokafoka
Anachukia: Wanyama wadogo wanapochezea mkia wake ili kuona atafanyaje

Tazama Video za Anko T Kupaka Rangi

Ngedere

Ngedere ni nyani kwa nje, na mfanyabiashara kwa ndani. Ana kibanda cha kuuza matunda sokoni lakini ana mipango mikubwa ya kukuza biashara yake. Anapenda kufanya utani na hachukulii maisha kwa uzito sana. Hii humsababishia kuingia kwenye matukio ya hatari sana!

Jina: Ngedere
Miaka: 28 (miaka ya nyani)
Familia: Kaka na dada wengi sana
Anachopenda: Kuchezea akili za watu na kula pilau!
Anachochukia: Mkia wake ukibanwa kwenye mlango
Siri kubwa: Alimwandikia Sungurita barua ya mapenzi

Tazama Video za Ngedere Kupaka Rangi

Toto Tembo

Ni mwenye kufikiri, kujali na mkarimu – huyo ndo Toto Tembo! Ni tembo mdogo mwenye kupenda kujifunza zaidi kama watoto wa Ubongo Kids. Pia ni mwerevu sana katika mambo ya fedha, na anapenda kuweka akiba ya maboga yake na kupanga bajeti kwa kila matumizi.

Jina: Toto Tembo
Miaka: 9
Familia: Baba (Senior Tembo)
Anapenda: Kupiga sarakasi za kichwa
Anachukia: Pale anaposhindwa kukumbuka kitu
Siri kubwa: Huwa anajaribu kuongea kama Mama Ndege pale ambapo hakuna mtu anayemuangalia.

Tazama Video za Toto Tembo Kupaka Rangi

Mzee Kigo

Mzee Kigo hapo mwanzo alikuwa ni mzee wa mjini, akifanya kazi ofisini. Lakini hakufurahia uchafu, kelele na maisha ya shughuli nyingi ya mjini, hivyo akarudi kijiji cha kokotoa kuanza kilimo. Ni mzee mwenye busara, mkarimu na mwenye taarifa za kuvutia – si jambo la kushangaza kwamba watoto humfuata pale wanapohitaji ushauri.

Jina: Mzee kigo
Miaka: 65
Familia: Mpwa wa kike na wa kiume ambao wapo mjini
Anachopenda: Kufuma kofia kwa ajili ya watoto njiti
Anachukia: Panya wanapokula mazao yake
Siri kubwa: Hajui kuendesha baiskeli

Tazama Video za Mzee Kigo Kupaka Rangi

Marafiki Wanyama

Marafiki Wanyama
cloth cloth
Wa Pink Wa Pink
Wa Bluu Wa Bluu
Kaka Kobe Kaka Kobe
Bundi Bundi
Da Chura Da Chura
Sungura Sungura
Senior Tembo Senior Tembo